Header Ads

WENGER AMUOMBA MOURINHO RADHI, ASEMA YEYE HAPENDI UGOMVI

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror na
kituo cha televisheni cha Telefoot,
Wenger amesema watu wametia sana
chumvi katika tukio lililo tokea kati yake
na Mourinho wikiendi iliyopita  na
kuupa uzito mkubwa ambao pengine
isinge stahili.
"Watu wamelikuza sana jambo hilo,
lakini pia nadhani nisinge paswa kufanya
vile nilivofanya kwa kuwa siyo siyo picha
nzuri katika mpira.
"Siku zote sipendezwi na hali yoyote ya
uhasama na kwa kutambua hilo, naomba
msamaha kwa kitendo nilicho kifanya
kwa kocha mwenzangu, Mourinho. Hali
ya hasira humtokea mtu yeyote. Lakini
pia ikumbukwe sikuingia katika eneo la
Mourihno kama ambavyo watu
wanasema"
Mpaka sasa bado shirikisho la kandanda
nchini Uingerza FA, halijasema
litachuakua hatua gani dhidi ya Wenger
na mwenzake Mourinho.

No comments

Powered by Blogger.