Header Ads

MBWA WAKUTWA WAKISHAMBULIA MABAKI YA MWILI WA BINADAMU - SONGEA

MIFUPA ya masalia ya binadamu wa jinsia ya kiume ambaye hakuweza kufahamika jina na kukadiliwa kuwa na miaka (30) yamegundulika na Zaujia Pilly (70) mkazi wa kijiji cha Lupapila
wilaya ya songea mkoani
Ruvuma wakati akienda kuchimba dawa za kienyeji baada ya kuwaona mbwa wakishambulia sehemu za mabaki hayo.

Akiongea na MTANDAO HUU ofisini kwake jana Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio
hilo limetokea oktoba 26
mwaka huu majira ya saa 9:45 alasiri huko
katika kijiji cha Lupapila
mtaa wa Mahinya kata ya Subira nje kidogo
ya manispaa ya Songea.

Alisema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio kwenye msitu wa uwanja wa
ndege ilikutwa mifupa ya binadamu wa jinsia ya kiume ikiwemo fuvu la
Kichwa, Mbavu, Mikono na Miguu wakati sehemu ya kiuno na mapaja ikiwa imeharibika vibaya.

Alifafanua kuwa mabaki ya mwili huo yaligunduliwa na Zaujia Pilly
wakati akienda kuchimba dawa za kienyeji kwenye msitu huo ghafla
aliwaona Mbwa wakifukuzana kugombania mabaki ya mwili wa binadamu.

Alieleza zaidi kuwa Zaujia baada ya
kugundua tukio hilo alitoa
taarifa katika uongozi wa serikali ya Mtaa na kisha taarifa zilipelekwa katika kituo kikuu cha polisi cha songea mjini ambako baadaye polisi walifika eneo la tukio wakiwa wameongozana na Daktari
kutoka hospitgali ya Mkoa wa Ruvuma ambaye aliyafanyia uchunguzi mabaki ya mwili huo na kubaini kuwa marehemu alikuwa amepigwa na kitu kizito kichwani kwenye eneo la kisogo kilichopelekea kifo chake.

Kamanda Msikhela alisema kuwa kufuatia tukio hilo hakuna mtu yeyote anayehusishwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma linaendelea kufanya uchunguzi wa kina juu ya kifo hicho.

No comments

Powered by Blogger.