Header Ads

MAHAKAMA KISUTU YAMZUIA DAVIDO "KUPERFORM" TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2014 - DAR


Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es
Salaam imemzuia msanii kutoka Nigeria, Adedeji
Adelek maarufu kama ‘Davido’ kuperform katika
tamasha la Fiesta linaloandaliwa na Clouds Fm na
Prime Promotion, October 18,2014.
Amri hiyo imetolewa jana (October 17) na hakimu
mkazi wa mahakama ya kisutu , mheshimiwa D.
Kisoka kufuatia maombi ya dharura
yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Times Fm
Radio na Times Fm Promotion.
Times Fm Radio na Times Fm Promotion
walipeleka maombi ya dharura mahakamani hapo
wakiitaka mahakama kumzuia msanii huyo
kuperform katika tamasha hilo kwa kuwa licha ya
BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) kukataa
kutoa kibali cha msanii huyo kwa maelezo kuwa
tayari alikuwa ameshachukuliwa kibali cha
kuperform nchini November 1 kwenye tamasha
lililoandaliwa na Times Fm Radio, Clouds Fm na
Prime Times Promotion waliendelea na taratibu
zote bila kujali zuio hilo la BASATA.
Times Fm Radio na Times Fm Promotion
waliiomba mahakama kuidhinisha madai yao dhidi
ya Clouds Fm, Prime Promotion na mkurugenzi
wa kampuni inayomsimamia Davido, HKN Music.
Madai hayo ni pamoja na kulipwa fidia ya
gharama na usumbufu waliosababishiwa na
walalamikiwa kadiri Mahakama itakavyoona inafaa.
Mahakama imetoa amri kuwa msanii huyo
amezuiwa kufanya onesho hilo October 18,2014
hadi pale ufumbuzi wa kesi hiyo utakapopatikana
mahakamani hapo.
Awali, Davido alisikika katika matangazo ya Times
Fm Radio akieleza kuwa atakuja Tanzania
November 1 kwa ajili ya kufanya onesho
linaloandaliwa na kituo hicho cha radio lililopewa
jina la ‘The Climax’.

NA TIMESFM.CO.TZ

No comments

Powered by Blogger.