MATOKEO: SIMBA NA YANGA MAPUMZIKO MABAO NI 0-0
Mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga, uwanja wa Taifa ni half time si Simba wala Yanga aliyeona
mlango wa mwenzake.
Dk 80, Hadi sasa Yanga
imepata kona 3,
halikadhalika Simba 3
Dk 79, Okwi anaingia eneo
la hatari lakini mabeki wa
Yanga wanaokoa na kuwa
kona, anaichonga lakini
haina matunda.
Dk 77, Manyika anafanya
kazi ya ziada kuokoa
shuti la Coutinho
aliyekuwa peke yake
akimtazama.
Dk 75 Coutinho anapewa
pasi nzuri kutoka kwa
Jaja, lakini anashindwa
kuifanyia kazi
Dk 74, Okwi analambwa
kadi ya njano baada ya
kumfanyia madhambi Juma
Abdul.
Dk 73, Jaja yeye na
Manyika, lakini napiga
mpira mkubwaaa....
Dk 72, Ngassa anaingia
ndani ya eneo la hatari
baada ya kupokea pasi
safi ya Coutinho, lakini
Manyika anatoka na
kuuwahi.Dk 68, Yanga
wanamtoa Niyonzima na
nafasi yake inachukuliwa
na Simon Msuva
Dk 67, Chanongo anapiga
mpira unagonga mwamba,
hata hivyo mwamuzi anasema
kablaya kupiga alikuwa
ameotea.
Dk 64, Mkude anatolewa
uwanjani kabisa, taarifa
zinaeleza amekimbizwa
hospitali kutokana na
kuteguka bega.
Dk 61, Pierre Kwizera
raia wa Burundi anaingia
kuchukua nafasi ya Mkude
Dk 60, Kiemba anapiga
kichwa safi lakini kidogo
tu linatoka.
Dk 54, Mkude anaumia na
kutolewa nje....
Dk 47, Okwi anapiga shuti
kali lakini linawababatiza
mabeki
MAPUMZIKO:
Dk 45+1, Ngassa, Hassan
Isihaka wanalambwa kadi ya
Njano, baada ya Ngassa
kumkita Isihaka ikiwa ni
maa ya pili kucheza rafu
hiyo. Lakini Isihaka
anapata adhabu kutokana na
kumsukuma Ngassa.
Dk 38, Simba wanamtoa
Ndemla na nafasi yake
inachukuliwa na Shabani
Kisiga
Dk 31, Okwi anaingia
ndanilakini Dida anadanya
kazi ya ziada kuokoa hatari.
Dk 29, Yanga wanapata kona
lakini kichwa na Oscar
hakikulenga lango
Dk 20, Coutinho anagongana na
Kiemba, anatolewa nje kutibia
baada ya kuchanika, lakini
anarudi uwanjani
Dk 18, Okwi anatuliza kifuani
mbele ya Juma Abdul, anaingia
vizuri mbele ya Cannavaro na
kupiga shuti kali, linatoka
juu kidogo tu ya lango la
Yanga...ilikuwa hatari.
Dk 17:36, Coutinho anapiga
shuti lakini Manyika anatoka
na kulidaka vema.
Dk 17 Okwi anatengenezewa na
Shabalaka anapiga shuti kali
linatoka nje kidogo.
Dk 13, Jaja anatuliza mpira
katikati ya mabeki ya Simba
na kuupira kiufundi, lakini
Manyika anashituka na
kuudaka.
Dk 6, Jaja anapiga kichwa
lakini kinatoka nje kidogo ya
lango la Simba.
Dk 4 Okwi anaingia na
kujaribu lakini shuti lake
Post a Comment