Header Ads

ANCELOTTI AJA JUU KWA KUFANANISHWA NA MOURINHO


MENEJA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amedai
hajawahi kufananisha mafanikio yake katika klabu
hiyo na ya kocha Jose Mourinho. Kocha huyo wa
zamani wa Paris Saint-Germain alichukua nafasi
ya Mourinho mwaka 2013 baada ya kocha huyo
kuisaidia timu hiyo kushinda taji la La Liga,
Kombe la Mfalme na Kombe la ligi katika miaka
mitatu aliyokuwepo Santiago Bernabeu. Hata
hivyo, inadaiwa aliondoka katika klabu hiyo kwa
utata kufuatia taarifa za kutoelewana na baadhi ya
wachezaji wa kikosi cha kwanza na kushindwa
kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa
Ulaya. Ancelotti alionekana kufikia mafanikio hayo
katika msimu wake wa kwanza kwa kuwafunga
mahasimu wao Atletico Madrid katika mchezo wa
fainali huku pia akishinda Kombe la Mfalme na
Kombe la Ligi. Matokeo hayo yanafanya wawili
hao kulinganishwa mafanikio yao katika timu hiyo
lakini Ancelotti amejitoa katika ulinganyisho huo
na kudai kuwa yeye anajaribu kufanya kazi yake
kila siku katika ubora. Ancelotti amesema
hajawahi kulinganisha mafanikio yake na
Mourinho katika klabu hiyo kwnai ana mambo
mengi ya kufikiria huku akijaribu kuisaidia timu
hiyo iweze kufanya vyema zaidi.

No comments

Powered by Blogger.