Header Ads

MCHEZAJI AFARIKI AKIJARIBU KUSHANGILIA BAO KAMA KLOSE - INDIA

MCHEZAJI AFARIKI AKIJARIBU KUSHANGILIA
BAO KAMA KLOSE
MWANASOKA amefariki dunia baada ya
kuanguka vibaya aliporuka samasoti
kushangilia bao katika mchezo wa Ligi Kuu
ya jimbo la Mizoram nchini India.
Peter Biaksangzuala amefariki akiwa hospitali
Jumapili baada ya kuangukia kichwa chake
aliporuka samasoti kushangilia bao
aliloifungia Bethlehem Vengthlang FC - klabu
yenye maskani yake Kaskazini Mashariki kwa
jimbo la Mizoram.
Mchezaji huyo aliyekuwa ana umri wa miaka
23 alifunga bao hilo dakika ya 62
kuisawazishia timu yake dhidi ya Chanmari
West FC Jumanne katika mchezo wa Ligi na
akataka kushangilia kwa staili ya mfungaji
bora wa kihistoria wa Kombe la Dunia,
Miroslav Klose.

Biaksangzuala alikosea katika kuruka kwake
na akapigiza kichwa chini, kabla ya kupatiwa
huduma ya kwanza uwanjani na kisha
kutolewa nje kwa machela.
Biaksangzuala alikimbizwa katika hospitali ya
Aizawl Civil ambako vipimo vya CT
vilionyesha amepata madhara makubwa kwa
undani na mara moja akahamishiwa chumba
cha wagonjwa walio chini ya uangalizi
maalum.
Chanzo kimesema: "Alijaribu kushangilia
kama Mjerumani Klose, lakini akakosea kwa
bahati mbaya. Alikaa hospitali kwa siku tano,
lakini madaktari hawakufanikiwa kuokoa uhai
wake,".
Taarifa nchini India zinasema kwamba
Biaksangzuala alichangia macho yake wakati
akiwa amelazwa hospitali.
Kwa ajili ya kumbukumbu ya kiungo huyo,
Bethlehem Vengthlang FC imeamua
kuipumzisha jezi namba 21 na Chama cha
Soka Mizoram kimetoa taarifa katika Ukurasa
wake maalum wa Facebook.

No comments

Powered by Blogger.