SMS NZURI ZA MAPENZI SOMA MTUMIE NA UMPENDAE
Najiuliza kila leo hivi ni mimi tu kimeo katika
dunia hii ya leo maana kila leo nayempata
huishia kunipa ahadi kila leo, mpenzi kila siku
waniaidi mara nitakupa leo mara kabla ya
machweo, hivi ni lini utanipa jibu la uhakika
nakunipa mapenzi ya uhakika nipate farijika?
Nakupenda mpenzi.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Hakika mtoto umeumbika mithili ya malaika
japo mbinguni sijafika lakini nauhakika kwa
kila mwanaume aliyeumbika na kukamilika
akikuona lazima udenda utamtoka, naomba
japo yako dakika nipate kukueleza moyoni
yaliyonifika kwani siwezi tena kuficha jinsi
navyokupenda, nakupenda amini kwako
nimefika!
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Nakupenda dear, amini moyoni umeniingia
ndiyo maana mimba nikaamua kukubebea
pasipo kunioa hakika mahaba yako yanifanya
nijione malkia katika hii dunia! Nakupenda
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ukweli lazima nikwambiye kwa kuwa sina
kimbilio nakupenda kijana mwenzio sijui
kwanini hutaki kukisikia changu kilio,
namwomba Mungu kila kukicha usikiye changu
kilio, nakupenda na kama kukueleza hili
nakukosea nisamehe kwani si langu
kusudio,luv u mwaah.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mhh kweli wewe ni mtaalam, unayejua
kuitumia yako kalamu kila nikuonapo hupata
hamu, hujihisi kupoteza fahamu, naomba
ufahamu wewe ndio wangu mtaalam!
Nakumiss
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kweli wewe ni mpishi! Umahiri wako unaanza
kwenye ukunaji nazi hadi upakuaji.
Upekechapo ndizi za mtori mimi huwa hoi.
Nakupenda mpenzi.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ooh My . . . . Hivi ni kweli umebanwa na kazi
au unaniwekea pozi? Mawasaliano yalikuwa
hayaishi tulipolianza letu penzi, leo si simu
wala sms nizipatazo toka kwako mpenzi,
hakika hunipendi siku hizi, enewei sina jinsi,
zaidi ya kumshukuru mwenyezi!
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mmh! Nakumbuka siku ya kwanza maneno
matamu uliyoniambia, ahadi kede ulinipatia,
nakunifanya nijione malkia katika hii dunia,
lakini leo umenibadilikia au kukupa penzi
nimekosea?
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Honey hivi unakumbuka? Ahadi uliyonipa,
mwisho wa mwezi ukifika pesa utanipa,
nitatuwe matatizo yaliyonifika, la azizi
nakukumbusha tarehe zimefika, na tatizo
langu bila wewe haliwezi tatulika! Luv u
mwaah.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mpenzi hakika ningekupa ila tarehe mbaya
zimefika hali ya hewa imechafuka, vumilia
wikiendi ijayo nitakupa, usiwe na pupa, mbivu
zako nitakupa hakuna mwingine wakumpa, luv
u.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Thamani ya Mapenzi yako nikubwa kwangu,
haifanani nachochote kwenye huu ulimwengu,
sina budi kumshukuru mungu, kwa kunijaalia
mpenzi mwema unaejali hisia zangu,
USICHOKE KUNIPENDA MPENZI
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Dhamira kuu ya Moyo wangu ni Mapenzi,
kukupenda kwa dhati bila kipingamizi, kuishi
nawewe kihalali kwa kudra za wazazi, Nipende
nikupende Tudumishe Mapenzi. "NAKUTAKIA
MCHANA MWEMA MPENZI WANGU"
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kwa kawaida busu la mafanikio hubusiwa
usoni, busu la amani hubusiwa mashavuni,
busu la upendo hubusiwa mdomoni, busu la
mapenzi hubusiwa shingoni, Je wapi nikubusu
ili ulale kwa raha sweet ?
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Naapa abadani penzi langu sitalitoa asilani
ingawa upo mbali nami, nakupenda amini
kwako nimefika, nitunzie langu penzi wasije
niibia washenzi.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Hakikisho la mapenzi: . . umeingia moyoni
mwangu kukutoa itakuwa ngumu sana,wajua
moyo huwa unafunguliwa mara moja hasa kwa
ile true love . . .
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Leo ni zaidi ya mwezi toka tumeyaanza yetu
mapenzi na kila kukicha nakuota kwenye njozi
ukinipa majambozi na huishi uchokozi, sijui
lini nitaacha hizi njozi kwa kunipa laivu lako
penzi, nakupenda mpenzi
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Sijui nini chakukukwambia furaha moyoni kila
saa yanijia tangu ulivyoniambia mimba ndiyo
ishaingia hivyo mtoto nikaye nikimtarajia,
nakupenda dear hakika wewe pekee ndiye
wangu malkia!
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Naamini uatakuwa umerejea kwenye yako
makazi na umechoka na kazi, tafadhali badili
yako mavazi , bafuni ingia upate maji
kujimwagia, natamani kuja kukusaidia mgongo
kuusugua na chakula kukuandalia lakini siku
haijawadia, nakupenda dear!
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Nawa kubali xana
ReplyDelete