Header Ads

Bingwa wa tenisi akerwa kuitwa ''kaka'.

Serena Williams
Bingwa wa mchezo wa tenisi kwa upande wa akina
dada duniani Serena Williams amekosoa matamshi
aliyoyataja kuwa ya kibaguzi na kutojali ujinsia
yaliotolewa na rais wa shirikisho la Tenisi nchini
Urusi Shamil Tarpischev dhidi yake na dadaake
Venus Williams.
Katika mazungumzo yake Tarpischev aliwaita kina
dada hao wawili kama ''kaka wawili'' .
Shamil Tarpischev
Hatahivyo afisa huyo alipigwa faini ya pauni 15,500
na kupigwa marufuku ya mwaka moja kwa kutoa
matamshi hayo aliyoyataja kama ya mzaha.
''Nadhani matamshi hayo yamejaa ubaguzi na
hayajali'' alisema Wiliiams.
''Sikuyapendelea hata kidogona nadhani watu
wengi pia hawakuyapendelea''.
matamshi ya Bwana Tarpischev pia yalishtumiwa
na shirikisho la mchezo wa Tenisi duniani WTA
pamoja na shikisho la mchezo huo nchini
marekani USTA.

BBC

No comments

Powered by Blogger.