Header Ads

NAHODHA BAFANA, ORLANDO PIRATES AUAWA KWA RISASI


KIPA wa timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ na klabu ya Orlando Pirates, Senzo Meyiwa (pichani) amepigwa risasi na kufariki dunia, Polisi nchini hapa imethibitisha jana.

Jeshi la Polisi imethibitisha mlinda mango huyo mwenye umri wa miaka 27 alithibitika kufa alipofikishwa katika hospitali East Rand, huko Gauteng.

Taarifa rasmi za shambulizi lake bado hazijapatikana na ofa nzuri imetangazwa kwa yeyote atakayetoa maelezo.

Nahodha huyo wa klabu na timu ya taifa, Meyiwa aliichezea Orlando Pirates juzi Uwanja wa Orlando wakishinda 4-1 kwenye Robo Fainali ya michuano ya mtoano ya Telkom dhidi ya Ajax Cape Town, Pumzika kwa amani Meyiwa.

No comments

Powered by Blogger.