Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro akana kuwepo mgonjwa wa Ebola
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
akana kuwepo mgonjwa wa Ebola
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Leonidas Gama amekanusha uvumi ulioenea kuwa yupomgonjwa wa Ebola mkoani humo.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa Redio Sauti ya Injili katika kipindi cha Dira kilichosikika
hewani baada ya saa mbili usiku wa Alhamisi, Oktoba 23, 2014, aliyemwambia kuwa zipo taarifa
kuwa yupo mgonjwa amegundulika na dalili za ugonjwa wa Ebola huko Shirimatunda, Mhe.
Gama amesema, “Msiwashitue watu bila sababu, hakuna Ebola”
Mwandishi: “ Sasa anaumwa nini huyo mgonjwa kama siyo Ebola?”
Gama: “Ana magonjwa ya kawaida. Unajua mtu unaweza kuwa na Malaria ukazidiwa, basi jibu la
haraka kwa sababu inawezekana ni mtu wa nje, watu wanasema Ebola… ni majibu mepesi.”
Mwandishi: “Sasa kwa nini apelekwe Shirimatunda
kama hana Ebola?”
Gama: “sasa hiyo waulize Waganga, lakini mimi
nina uhakika taarifa zao ni kwamba hakuna mtu
ana Ebola”
Mwandishi: “...taarifa ni kwamba kile kituo
wamekiandaa kwa ajili ya kuhifadhi wagonjwa wa
aina hiyo, na ndiyo maana wamemtoa moja kwa
moja kutoka Uwanja wa Ndege wakampeleka
Shirimatunda.”
Gama: “Hapana, si kweli. Usiwe na wasiwasi. Si
hata wewe ukitiwa wasiwasi kuwa una
kipindupindu, si kwamba ndiyo una kipindupindu?
Unajua suala la tahadhari siyo kwamba ndiyo ukweli. Ni tahadhari. Maana yake, unaweza ukachukua tahadhari kama kuna mtu ana wasiwasi. Kama unatiliwa wasiwasi kwamba huyu bwana anaumwa kipindupindu, lazima wamwangalie je, ana kipindupindu kweli? …kumwangalia kipindupindu siyo lazima awe na kipindupindu.”
★☆ MPEKUZI
Post a Comment