Header Ads

MAN UNITED WAHAHA DI MARIA ACHEZE DHIDI YA CHELSEA JUMAPILI

MAN UNITED WAHAHA DI
MARIA ACHEZE DHIDI YA
CHELSEA JUMAPILI

WINGA wa Manchester United, Angel di Maria Jumatano alikuwa Carrington kwa matibabu
katika siku yake ya mapumziko, katika jitihada za kocha Louis van Gaal kuhakikisha mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa dau la rekodi
anakuwa fiti kwa ajili ya mechi na Chelsea Jumapili.

Di Maria — tegemeo la Van Gaal kwa sasa kati ya nyota aliosajili, alitolewa wakati United ikienda sare ya 2-2 na West Brom katika
mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatatu, kabla ya kugundulika aliumia mguu.

Haijatolewa taarifa rasmi na klabu hiyo, lakini nyota huyo wa zamani wa Real Madrid alikuwa Carrington kufanyiwa Jumatano na
vyanzo vinasema mwanasoka huyo wa kimataifa wa Argentina yuko katika nafasi ya kucheza Jumapili Uwanja wa Old Trafford.

Aidha, Chelsea inatarajiwa kusafiri hadi Manchester bila mfungaji wao tegemeo Diego Costa na  Loic Remy wote ni majeruhi.

Pia, Man United, wakati huo huo itamkosa Nahodha wake, Wayne Rooney ambaye atakuwa anamalizia adhabu yake ya kadi iliyomfanya akose mechi tatu baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu dhidi ya West
Ham.

No comments

Powered by Blogger.