TANZANIA YAKATAA RASMI NDOA ZA JINSIA MOJA KWENYE AGENDA ZA MAENDELEO YA MILENIA
SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika
mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika
mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.
“tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy Amesema kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda ya watanzania na si agenda ya maendeleo.
Soma zaidi hapa; MICHUZI
Post a Comment