Header Ads

Wanajeshi saba wauawa na bomu Misri

Mlipuko
Maafisa nchini Misri wanasema kuwa takriban
wanajeshi saba wameuawa na wengine wanne
kujeruhiwa baada ya bomu lililokuwa limetegwa
kando kando ya barabara kulipuka katika mkoa wa
Sinai.
Mlipuko huo ulilikumba gari lao ambalo lilikuwa
likipiga doria katika eneo ambalo bomba la gesi
linapitia katika mfereji.
Kumekuwa na mashambulizi ya mara kwa mara
dhidi ya jeshi la Misri pamoja na miundo msingi
katika eneo la Sinai tangu rais Abdel fatah al Sisi
achukue uongozi wa taifa hilo mwaka 2013.

BBC

No comments

Powered by Blogger.