WENGER ATOBOA SIRI YA MAJERUHI YA OZIL
MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger
amebainisha kuwa Mesut Ozil alihisi tatizo katika
goti lake katika mchezo dhidi ya Chelsea lakini
aliendelea kucheza hivyo hivyo. Kiungo huyo
alicheza dakika zote tisini katika mchezo huo
waliofungwa mabao 2-0 lakini daktari wa
Ujerumani alimuondoa katika kikosi cha timu ya
taifa ya nchi hiyo baada ya kugundua kuwa
kiungo huyo amechanika msuli wa ndani la goti
lake ambao unaweza kumuweka nje kwa kipindi
cha miezi mitatu. Wenger amesema
anashangazwa na majeruhi ya wachezaji wake na
kukiri kuwa anapata wakati mgumu kwani
inaoenekana wachezaji wengi wenye majeruhi ya
muda mrefu wameyapata bila hata kuguswa na
mchezaji mwingine. Kocha huyo aliendelea kudai
kuwa Ozil alilalamika kusikia maumivu kidogo
wakati wa mapumziko na alimuambia daktari wao
amuangalie na kama kutakuwa na tatizo lolote
amuambie kwasababu tayari walikuwa nyuma kwa
bao moja hivyo alihitaji wachezaji wote wa safu ya
ushambuliaji. Wenger amesema
kinachomshangaza ni kuwa Ozil hakugongana na
mchezaji yeyote uwanjani, alikuwa akijaribu kutoa
mpira kwa mwenzake ndipo alipoumia. Kutokana
na majeruhi ya mara kwa mara yanayoiandama
klabu hiyo baadhi ya wadau wamekuwa wakihoji
mazoezi wanayopewa wachezaji hao lakini Wenger
mwenyewe ametetea na kudai kuwa ni suala la
bahati mbaya kwani wachezaji wake wengi
waliopata majeruhi hivi karibuni yalitokana na wao
wenyewe bila kuguswa.
Post a Comment