Majibu ya Jaji Warioba Katiba Mpya
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema muundo wa
Muungano uliopendekezwa kwenye Katiba
pendekezwa ‘una utata mkubwa’ hasa baada ya
kupunguza mambo ya Muungano na kwamba
kunaipa nguvu Serikali ya Jamhuri ya Muungano
kuwa Serikali ya Tanganyika.
Alisema muundo wa serikali mbili hauwezi
kuendelea kwa sababu haiwezekani kuwa na
serikali ya Jamhuri ya Muungano, isiyovuka bahari.
Akizungumza na NIPASHE ofisini kwake Oysterbay
jijini Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema pia
kwamba haoni kama Wazanzibari watakubali
kuipitisha Katiba pendekezwa kwa kuwa Ibara ya
294 inataka Katiba ya Zanzibar ifanyiwe
marekebisho ili iwiane na Katiba ya Jamhuri ya
Muungano.
Alisema wananchi wa pande zote walieleza namna
kero za Muungano kwa kina na ndiyo maana Tume
yake ikapendekeza muundo wa Serikali tatu kama
mwarobaini wa matatizo hayo.
Bofya kusoma zaidi; NIPASHE
Post a Comment