Header Ads

DIEGO COSTA AWEZA KUCHEZA DHIDI YA MAN UNITED JUMAPILI - MOURINHO

MOURINHO ASEMA DIEGO COSTA AWEZA CHEZA DHIDI YA MAN UNITED JUMAPILI

KOCHA Jose Mourinho ameghairi kumuweka benchi mshambuliaji Diego Costa katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United Jumapili.

Mshambuliaji huyo wa kati wa Hispania, amekosa mechi mbili zilizopita katokana na maumivu ya nyama na wiki hii alipelekwa hospitali kwa tiba ya tatizo hilo.

Lakini Mourinho, ambaye amethibitisha Loic Remy atakuwa nje kwa wiki tatu zijazo kwa maumivu ya nyonga, amesema mshambuliaji wake huyo nyota ana nafasi ya kwenda Old Trafford.

Alipoulizwa leo iwapo Costa atacheza, Mourinho akasema; "Kuna nafasi, ana nafasi ndogo, Diego ana nafasi kidogo, sawa na Ramires na (John Obi) Mikel, Lakini Remy yuko nje na hatacheza. Hana nafasi," "Kila kitu kilichotokea (kwa Costa), Alikuwa majeruhi kama kawaida- hiyo ilikuwa ni nyama".

Ilibidi aende hospitali kwa matibabu, tatizo ambalo tusingeweza kulitatua bila kuwa hospitali kwa usiku mmoja- hiyo ilikuwa kabla ya kucheza na Maribor,"amesema.

No comments

Powered by Blogger.