Header Ads

UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KAHAMA HUWENDA UKAINGIA DOSARI

ZOEZI la kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea uongozi wa ngazi mbalimbali wa srikali za Mitaa Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga huenda isifanikiwe kutokana na baadhi ya Wananchi katika kata za Mwendakulima na Mhongolo kugoma kuchukua fomu kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja kujiuzulu kwa viongozi wao.

Katika kata ya Mwendakulima Wananchi wamegoma kuchukua fomu hizo mpaka uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama kumuondoa Mtendaji wa kata hiyo Cesilia Clement ambaye wanamtuhumu kwa kutosimamia shughuli za maendelea ipasavyo katika kata hiyo iliyopo jirani na Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.

Pia katika kata ya Mhongolo Mwenyenyekiti wa CCM wa Kata hiyo John Masalu ameamua kujiuzulu kutokja na sababu mbnalimbali ikiwemo tangia kukaa kwa kikao cha kamati use siasa  ya Wilaya  tarehe 26/05/2014 na kutoa maamuzi ya kumsimamisha katibu wake amekuwa ashirikishwi kikamilifu katika mambo yanayohusu chama hicho.

Katika barua yake kwenda kwa katibu wa CCM Wilaya ya Kahama  ya tarehe 12/10/ 2014 nakala tunayo Mwenyekiti huyo alisema kuwa kwa sasa kumekuwa makundi makubwa ya chama hicho katika kata hiyo na kuongeza kuwa sasa ni kama ametengwa kwani ashirikishwi katika mambo yeyote ya chama hicho na nikamati tendaji tuu ndio inayohusika.

Pia Mwenyekiti huyo katika barua hiyo alisema kuwa kumekuwa na ugawaji wa kadi bubu za CCM katika kata hiyo kweatu ili watarajie kugombea udiwani  kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi wapate wapiga kura zao za maoni kwa maslahi binafsi na kuongeza suala hilo alilitolea taarifa katika ngazi husika lakini halikuweza kushughulikiwa.

Aidha alisema kuwa kadi hizo zimetia dosari katika kata hiyo na hivyo kuwagawa kwa kiasi kikubwa wapiga kura hali inayopelekea kata hiyo katika uchaguzi ujao wa Madiwani kubakli kushikiliwa na chama pinzani cha Chadema kama ilivyo hivi sasa.

Mwenyekiti huyo pia alitoa wasiwasi wake kwa uongozi wa Chama cha Mapinduzi kuhakikisha kuwa wanafanya uchaguzi wa haraka wa kumpata mwenyekiti mpya wa kata ya Mhongolo kwani uchaguzi huo utakuwa mgumu kufanyika kutokana na kutokuwa na mwenyekiti.

Kutokana na matatizo hayo kamati ya siasa yaChama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama imeamua
kukaa kikao kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kutatuamatatizo hayo husuisani la kukataliwa kwa
Mtendaji wa Kata ya Mwendakulima hali iliyfanyawananchi kukataa kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi katika serikali za mitaa.


Source: KIJUKUU CHA BIBI K - BLOG

No comments

Powered by Blogger.