Header Ads

Katibu wa CHADEMA akipiga chini chama hicho kwa siasa za kidikteta...Ajiunga CCM


Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Mtera, Lameck
Lubote ametangaza kukihama chama hicho na
kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
kusema amechoka na siasa zilizojaa udikteta wa
viongozi wake.
Alisema hayo mbele ya waandishi wa habari mjini
hapa jana huku akiwa amefuatana na
mwanachama mwenzake ambaye naye amehama
Chadema, Gwakisa Mwakasendo.
“Nimechoshwa na ninakerwa na siasa za kitoto
zinazofanywa na Chadema pamoja na chama
hicho kuwa na maandamano yasiyokwisha,”
alisema.
Pia alisema viongozi ndani ya chama hicho
wamekuwa na maamuzi ya kidikteta ambayo yana
maslahi ya wachache kitu ambacho si sawa sawa.
Lubote alisema Chadema imejaa vituko ikiwemo
Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe
kuhamasisha maandamano huku yeye akiondoka
kwenda Afrika Kusini.

Bifya kusoma zaidi Mpekuzi

No comments

Powered by Blogger.