Header Ads

KINACHOWAPONZA WEMA, KAJALA

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu
‘Madam’ .Kudhihirisha kwamba
wameshibana, kuna wakati KAMA walivyo
Wema Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel kwa
sasa ndivyo walivyokuwa Wema na Kajala
Masanja miezi kadhaa iliyopita.Wema na
Kajala walikuwa mashosti wa kufa mtu,
walishibana na kupeana siri zao zote hususan
zile za ndani kabisa. Wema aliamua kujitolea
Sh. Mil 13 kulipa faini ambayo ilimnusuru
Kajala kuswekwa gerezani.Baadaye walikuja
kutofautiana, kila mtu akaishi kivyake.
Yakazungumzwa mengi
kuhusu chanzo cha ugomvi wao lakini pointi
ya msingi ni kupishana kauli kibinadamu
kama watu wengine wanavyoweza
kutofautiana na kupatana.
Kwa upande wao suala la kupatana limekuwa
zito, ugomvi wao haufiki tamati hukukila
kukicha ni malumbano ambayo yanawagawa
mashabiki.

Mastaa wa filamu Bongo, Wema Sepetu
‘Madam’ na Aunt Ezekiel wakipozi.Tatizo
kubwa linalochagiza ugomvi wao ni
mitandao ya kijamii, kumezuka makundi
ambayo yamekuwa yakitumia utabiri wao
wanaoufahamu wenyewe kuzidi kuchochea
ugomvi uliokuwepo kati ya mastaa hawa
wawili na wengine wakitumia matusi mpaka
ya nguoni kutukana wa upande wa Wema na
Kajala.
Makundi hayo ndiyo yamekuwa chachu
kubwa ya bifu lao na kuzidisha mapambano
kati ya mastaa hawa ambao naamini
wanapendana sana, sitaki kuamini kabisa
kama Wema hampendi Kajala, na sitaamini
kama Kajala hampendi Wema.

BOFYA KUSOMA ZAIDI

No comments

Powered by Blogger.