Header Ads

CHELSEA KUMKOSA DIEGO COSTA LIGI YA MABINGWA - MOURINHO


CHELSEA KUMKOSA
DIEGO COSTA LIGI YA MABINGWA,
MOURINHO ASEMA KURUDI UWANJANI
LABDA NOVEMBA KATIKATI

MSHAMBULIAJI Diego Costa ataukosa
mchezo wa Jumanne wa Ligi ya Mabingwa
Ulaya, timu yake Chelsea ikimenyana na NK
Maribor Uwanja wa Stamford Bridge,
amesema kocha Jose Mourinho.
Costa alikuwa nje ya kikosi cha Chelsea jana
kikishinda 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika
Ligi Kuu ya England na ataendelea kupata
tiba kwa muda.
Mpachika mabao huyo wa zamani wa Atletico
Madrid aliumia akiichezea timu yake ya taifa
Hispania na Mourinho amesikitishwa mno na
kumkosa nyota wake huyo mkali wa mabao.
Diego Costa atakosekana Chelsea ikicheza
Ligi ya Mabingwa Ulaya keshokutwa
"Baada ya mechi na Arsenal akaenda timu ya
taifa, akacheza mechi mbili kubwa na
amerudi akiwa na hali ambayo hawezi
kucheza,"amesema Mourinho.
"Nafikiri atakuwa katika hali nzuri katikati ya
Novemba kurejea katika timu ya taifa.
Tutakuwa makini mno juu yake. Atacheza
kwangu atakapokuwa huru baada ya kumaliza
majukumu ya timu ya taifa,"amesema.

No comments

Powered by Blogger.