Header Ads

CHANZO CHA AJALI YA LORI LA MAFUTA MBAGALA, NA KILICHOSABABISHA MOTO KUWAKA

WATU wa tatu wamefariki dunia huku wengine 16
wakijeruhiwa katika ajali ya lori la mafuta
lililopinduka katika mzunguko wa Mbagala Rangi
tatu jijini Dar es Salaa jana usiku.
Ajali hiyo ya lori la mafuta ilitokea wakati lori hilo
ambalo halijafahamika ni mali ya kampuni gani
kupinduka wakati dereva wake akijaribu kulikwepa
gari lingine lililokuwa mbele yake. Akisimulia
chanzo cha ajali hiyo mmoja wa mashuda
amesema mara baada ya gari hilo kupinduka
dereva alitoa tahadhari kwa vijana waliofika eneo
hilo kuwa waache kuchota mafuta hayo na
endapo wakifanya hivyo wathithubutu kuwasha
moto au kugusa betri lakini ghafla palitokea mtu
aliyewasha mshumaa jirani.
Kuwashwa kwa mshumaa huo kulisababisha
moto kulipuka na hatimaye moto kufika hadi
katika gari hilo na kuunguza watu waliokuwa
wakichota mafuta. Mmoja wa waliokuwa
wakichota mafuta alikimbilia baa ya United State
kutafuta maji ajizime moto na kusababisha moto
kulipuka tena eneo hilo la bar na mtu mwingine
alikimbilia eneo la gesti kutafuta maji nae
akasababisha moto katika magodoro na
kuiteketeza kabisa nyumba hiyo ya wageni iliyo
na vymba 32.
Mbali na nyumba hiyo ya wageni pia moto huo
uliteketeza kabisa mali katika vibanda vinne vya
biashara vilivyokuwa eneo hilo na pikipiki. Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic
alifika katika eneio la tukio na kutoa onyo kwa
wananchi kusogelea magari ya mafuta yanapo
anguka.

No comments

Powered by Blogger.