Header Ads

Jay Z na Beyonce Wakata Watu Midomo Kwa Kurudia Kiapo Cha Ndoa

Rapper Jay Z na mkewe Beyonce Knowles wameamua kuzama tena kwenye kina kirefu cha maisha ya ndoa baada ya siku kadhaa za misukosuko na tetesi za kuachana.

Kwa mujibu wa jarida la ‘People’, mastaa hao ambao ndoa yao imetimiza miaka sita, wamerudia kiapo cha ndoa hivi karibuni.
“Walikuwa na matatizo makubwa. Lakini wameyatatua na wamerudia kiapo chao cha ndoa.” Chanzo hicho kimeliambia jarida la People.

Katika majira ya kiangazi wakati wakiendelea na ziara yao waliyoipa jina la ‘On The Run Tour’ kulikuwa na tetesi za ugomvi na kutengana vyumba wakati wa ziara hiyo lakini walipokuwa Paris, Ufaransa, Jay Z alitoa ujumbe mzuri kwa mashabiki kuhusu uhusiano wao.
“We love Paris. It’s special to us because we got engaged here, and this is where Blue Ivy was conceived.”

Jay Z na Beyonce wameendelea kushare picha za familia yao kwenye mitandao ya kijamii na wanaelezwa kuingia studio kuandaa album yao ya pamoja inayotarajiwa kutoka mwaka 2015.

No comments

Powered by Blogger.