Header Ads

Kukamatwa kwa Chidi: Nzowa atoa onyo kali

Kufuatia tukio la Msanii wa muziki Chidi Beenz kukamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aonya vijana kutokujihusha na dawa hizi kabisa.

Kamanda Nzowa amesema kuwa tukio la kukamatwa kwa msanii huyu mkubwa, ni nafasi ya jamii na vijana kujifunza na kuachana na dawa hizi ambazo madhara yake kwa jamii ni makubwa.

Chidi baada ya upekuzi alipatikana na kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi, tukio ambalo limeendelea kuzua maoni tofauti kutoka kwa watu mtandaoni wakati huu ambapo anasubiri hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yake.

No comments

Powered by Blogger.