Header Ads

Hofu ya `Ebola` Tanzania


-Mmoja afariki na sita wawekwa karantini
-Sampuli zapelekwa Hospitali ya Muhimbili

Watu sita wakiwamo wahudumu watatu wa afya wa
hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema mkoani
Mwanza, wamewekwa chini ya uangalizi maalum
baada ya kumhudumia mgonjwa aliyefariki akiwa
na dalili za ugonjwa wa ebola.
Mtu aliyefariki alitajwa kuwa ni Salome Richard
(17), anayetoka katika kijiji cha Kahunda wilayani
Sengerema.
Akithibitisha kuwapo kwa hali hiyo Mganga
Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Wilaya ya
Sengerema, Dk. Mary Jose, alisema mgonjwa huyo
alifikishwa katika hospitali hiyo na ndugu zake
watatu akiwa na homa kali huku akitokwa na damu
sehemu mbalimbali za mwili wake.
Alisema vipimo vya mgonjwa huyo vimepelekwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
“Tulimpokea juzi saa 7 mchana kutoka katika kijiji
cha Kahunda wilayani hapa akiwa na homa kali
akitokwa damu mwilini, lakini kwa tahadhari
tulimweka wodi maalum peke yake akipatiwa
matibabu na ilipotimu saa 8 usiku alifariki dunia,”
alisema.
Alisema kutokana na tahadhari ya ugonjwa huo,
watumishi watatu wa idara ya afya na ndugu
watatu wa marehemu huyo, wamezuiliwa kwa
kuwekwa katika uangalizi maalum hadi matokeo ya
vipimo vilivyochukuliwa vitakaporejeshwa toka
Muhimbili.

Bofya kusoma zaidi; NIPASHE

No comments

Powered by Blogger.