Header Ads

HAIJAWAHI KUTOKEA, REFA NICOLAS AMLIMA KADI NYEKUNDU CAVANI KISA KUSHANGILIA KWA STAILI YA MTUTU WA BUNDUKI


HAIJAWAHI KUTOKEA,
REFA NICOLAS AMLIMA
KADI NYEKUNDU CAVANI
KISA KUSHANGILIA KWA
STAILI YA MTUTU WA
BUNDUKI

MSHAMBULIAJI Edinson Cavani jana alikuwa
miongoni mwa wachezaji watatu
walioonyeshwa kadi nyekundu wakati Paris St
Germain ikiitandika RC Lens mabao 3-1 katika
mchezo wa Ligue 1 Uwanja wa Stade de
France.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa
alipewa kadi hiyo na refa Nicolas Rainville,
baada ya kushangilia bao la mwisho la timu
yake kwa ishara ya kupiga bunduki, staili
maarufu kwa klabu ya Arsenal ya England.
Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi ameponda
maamuzi hayo ya utata akisema kwamba
kama adhabu zitatolewa kwa ushangiliaji wa
aina hiyo, ni mbaya kwa soka ya Ufaransa.
Mabao ya PSG yalifungwa na Cabaye dakika
ya 28, Maxwell dakika ya 33 na Cavani dakika
ya 55, wakati Lens pia ilipoteza wachezaji
wawili waliotelewa kwa kadi nyekundu,
Gbamin na Le Moigne, huku bao lao la kufutia
machozi likifungwa ma Coulibaly dakika ya
10.

No comments

Powered by Blogger.