Header Ads

HISPANIA YAZINDUKA KUFUZU EURO, YAUA 4-0 DIEGO COSTA AKIFUNGUA AKAUNTI YA MABAO YA KIMATAIFA HISPANIA

HISPANIA
YAZINDUKA KUFUZU EURO, YAUA 4-0
DIEGO COSTA AKIFUNGUA AKAUNTI YA
MABAO YA KIMATAIFA
HISPANIA imeichapa mabao 4-0 Luxembourg
katika mchezo wa Kundi C kufuzu Euro 2016
usiku jana ugenini.
Katika mchezo huo, ambao kipa Iker Cassilas
wa Real Madrid alipumzishwa akimpisha
David de Gea wa Manchester United, kiungo
wa Manchester City, David Silva alifunga bao
la kwanza dakika ya 27 kabla ya Paco Alcacer
kufunga la pili dakika ya 42.
Diego Costa, aliyepoteza nafasi za kufunga
kipindi cha kwanza, hatimaye akafungua
akaunti yake mabao timu ya taifa kwa bao la
dakika ya 69, kabla ya Juan Bernat aliyetokea
benchi kufunga la nne dakika ya 88.
Costa anafunga bao lake la kwanza kwa nchi
yake hiyo ya kuhamia baada ya dakika 515
za kuichezea bila kuifungia. Katika mechi
nyingine za Kundi C, Ukrine iliichapa FYR
Macedonia 1-0 bao pekee la Sydorchuk
dakika ya 45 wakati Slovakia iliichapa 3-1
Belarus.
Kundi G, Austria imeifunga 1-0 Montenegro,
Urusi imetoka 1-1 Moldova na Sweden
imeifunga 2-0 Liechtenstein.
Kikosi cha Luxembourg kilikuwa: Joubert,
Mutsch, Chanot, Martins Pereira/Turpel dk60,
Philipps, Janisch, Jans, Gerson, Holter, Da
Mota Alves/Payal, dk75 na Bensi.
Hispania: De Gea, Pique, Bartra, Jordi Alba,
Carvajal, Busquets, Iniesta/Bernat dk72, Koke,
Silva/Pedro, dk71, Alcacer na Costa/Rodrigo,
dk83.

No comments

Powered by Blogger.