Header Ads

MAHAKAMA YAAMURU KUKAMATWA KWA MAGARI YA NMB NA VODACOM - MBEYA


MAHAKAMA ya Wilaya ya Chunya,
Mkoani Mbeya, imetoa kibali cha
kukamatwa na kuuzwa kwa
magari matatu ya Taasisi ya
Kibenki ya NMB na  Kampuni ya
mawasiliano Vodacom Tanzania, ili
kulipa fidia ya shilingi milioni
86,553,700 kwa kosa la
kumsababishia mteja hasara
baada ya kuhamisha fedha kwenye
akaunti kwa kutumia huduma
ya  kibenki  ya njia ya simu bila
idhini yake.
Kesi hiyo namba 4 imefunguliwa
mahakamani hapo, Mei 13 mwaka
huu na mlalamikaji Mwanswa
Jonas dhidi ya Taasisi ya kibenki
ya NMB na kampuni ya Vodacom
Tanzania na mahakama hiyo
kutoa hukumu Oktoba 13 mwaka
huu kwa kutoa kibali cha kuuzwa
kwa magari hayo.
Akisoma shitaka hilo, hivi karibuni,
Kalani wa mahakama ya Wilaya ya
Chunya Izza Sheumu, mbele ya
hakimu wa Wilaya, Desdery
Magezi, alisema, Mei 13,2014 ,
mlalamikaji alibaini kupotea kwa
fedha zake zikiwa na thamani ya
shilingi milioni 6,553,700
zilizokuwa kwenye akaunti namba
6071600335 kupitia benki ya NMB.
Amesema, uchunguzi ulibaini kuwa
fedha hizo zilipotea baada ya
kuhamishwa kwa kutumia huduma
ya kibenki ya njia ya simu kutoka
akaunti namba 6071600335
kwenda kwenye namba ya
simu  ya mkononi ya Vodocom
0768 713668 bila ya idhini ya
mteja.
Amesema, imeelezwa kuwa wakati
zoezi hilo linafanyika mteja huyo
alisitishiwa huduma ya
mawasiliano kwa muda na
kwamba alipofuatilia kwenye ofisi
za Vodacom, alielezwa kwamba
asubiri huduma yake itarudishwa
kwani kunamatatizo ya kiufundi.
Amesema, mlalamikaji  huyo akiwa
katika harakati za kuweka kiasi
cha fedha cha shilingi milioni 16
kupitia kwenye akaunti yake iliyopo
katika benki ya NMB kabla ya
kuweka fedha hizo aliomba salio
na kuambia salio lake halitoshi
licha ya akaunti yake kudaiwa
kuwa na kiasi cha fedha  zaidi ya
shilingi milioni sita.
Amesema, alipofuatilia
alishangazwa kuelezwa kwamba
fedha hizo alizitoa yeye kupitia
namba yake ya simu ya mkononi
ya Vodocom jambo ambalo
alilipinga hivyo kuamua kupeleka
malalamiko yake kwenye ofisi za
wanasheria Tanganyika Law
Society na kesi hiyo kusimamiwa
na wakili wa kujitegemea,
Radlsaus Lwekaza, ambaye
aliiomba mahakama kusikiliza kesi
hiyo, Julai 24, mwaka huu.
Pia, imeelezwa kuwa wakili,
Rwekeza, aliiomba mahakama
kusikiliza kesi hiyo upande mmoja,
kwa kuelezea kwamba wadaiwa
wameamua kwa makusudi
kutohudhuria na kujitetea kwenye
kesi husika baada ya mahakama
kuhairisha kesi hiyo mara nyingi
bila ya wao kutokea licha ya
kupelekewa hati ya kuitwa.
Amesema, baada ya hapo kesi
ilisikilizwa upande mmoja,  na
mahakama hiyo kutoa hukumu
15/8/2014 ya kwamba mshitakiwa
namba moja ambaye ni NMB alipe
shilingi milioni 43, 272,750 na
Vodacom alipe milioni 43,272,750
ambapo mdai aliomba kukazia
hukumu baada ya siku 30 za rufaa
kupita na mahakama ilimkubalia
na hatimaye Oktoba 13 mwaka huu
mahakama ilitoa kibali kwamba
magari mali ya NMB na Vodacom
kuuzwa.
Mahakama hiyo, iliyataja magari
hayo kuwa ni gari namba T519
CHP Nissan Patrol nyeupe , T947
CVE Toyota Land Cruiser mali ya
Taasisi ya Kibenki ya NMB na gari
namba T388 CGW Nissan Hard
Bord mali ya kampuni ya
Vodocom.
Aidha, mahakama hiyo ilitoa kibali
kwa Kampuni ya Jagro Enterprices
limited, inayomilikiwa na Maulid
Hamis kukamata magari hayo.

No comments

Powered by Blogger.