Header Ads

BALOTELI AKUTANA NA BALAA LINGINE JANA AKIWA JIJINI MANCHESTER KISA KUMTISHIA DADA WA WATU ALIYEJARIBU KUPIGA PICHA GARI LAKE

Baada ya Baloteli kujiunga na klabu ya Liverpool akitokea AC Millan ya nchini Italy mwishoni mwa dirisha kubwa la usajili 2014/2015, aliagiza aletewe gari lake hilo kwa njia ya meli kutoka Italy kwenda Uingereza.

Wakati mtukutu Super Mrio Baloteli akisubiri adhabu kutoka kwa kocha wake, Brendan Rodgers kwa kosa la kubadilishana jezi na Beki wa Real
Madrid 'Pepe" Juma tano
iliyopita kabla mechi haijaisha, Baloteli amekutana na kisanga kingine dhidi ya maafisa wa polisi jijini Manchester baada ya kumtishia mwanamke
mmoja aliyekuwa akijaribu kupiga picha gari lake la kifahari akiwa njiani kuelekea kwa mama yake
jijini humo.

Baloteli alikuwa jijini Manchester ambako alikwenda kumsalimia mama yake anayefahamika
kwa jina la Rose Barwuah ambaye anaishi mitaa ya Wythenshawe jijini humo, lakini ghafla akiwa
njiani kuelekea kwa mama yake, alimuona mwana dada mmoja akiwa bize kupiga picha gari lake
aina ya Ferrari 12 Berlinetta ambalo gharama yake inakdariwa kuwa ni paundi 240,000 sawa na
milioni za kitanzania mia nne themanini (480,000,000).

Katika hali isiyotarajiwa, Baloteli alianza kumkemea dada yule huku akimtishia kumpiga makofi endapo angeendelea kufanya hivyo,
kitendo kilichomfanya dada huyo kwenda polisi kushitakiki kwa kutishiwa maisha na Baloteli.

Great Manchester Police (GMP), wamesema wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu suala hilo
kisha watamchukulia Baloteli hatua endapo atakuwa na hatia ya kutishia maisha ya watu.

Hilo linakuwa ni janga la pili kumpata Baloteli wiki hii ambaye anasubiri adhabu kutoka kwa kocha
wake Brenda Rodgers kwa kosa la kubadilisha jezi kabla ya mechi kumalizi katika mechi ya
Jumatano iliyopita ambayo Liverpool ilipigwa
magoli 3-0 dhidi ya miamba ya soka wa Hispania,
Real Madrid.

No comments

Powered by Blogger.