Header Ads

AMBASSADOR YA KAHAMA KUIPIMA YANGA KIWANGO JUMATANO

Kikosi cha Ambassador cha mjini Kahama kitakuwa mwenyeji wa Yanga katika mechi ya kirafiki
itakayopigwa Jumatano.

Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto ameviambia vyombo vya habari kuwa kweli mchezo huo utakuwepo.

“Ni kweli tuna mechi, itapigwa Jumatano na baada ya hapo ndiyo tutasafiri kwenda Bukoba, hiyo timu
inashiriki daraja la pili,” alisema Kizuguto.

Mechi hiyo itakuwa ya pili ya Yanga kirafiki kwa kuwa ilianza kucheza na
CDA ikiwa mjini Dodoma na kutoka nayo sare ya bila kufungana halafu ikasafiri hadi Shinyanga na kuifunga
Stand United kwa mabao 2-0.

Yanga iko katika maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar itakayopigwa wikiendi hii kwenye Dimba la Kaitaba, mjini Bukoba, Mechi hiyo itapigwa kwenye
Uwanja wa Kahama.

Source: SALEH JEMBE

No comments

Powered by Blogger.