Header Ads

Pinda atangaza rasmi kuwania urais

Dar es Salaam. Siyo tetesi tena. Sasa ni rasmi kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amekuwa akitajwa kuwania urais amethibitisha wazi kuwa
atagombea kiti hicho katika uchaguzi mkuu mwakani.

Alitoa uthibitisho huo juzi akiwa London, Uingereza ambako yuko katika shughuliza kikazi. Hatua hiyo inaondoa uvumi ambao umekuwapo kwa takriban miezi mitatu sasa kwamba naye tayari ameingia
katika kinyang’anyiro hicho.
Pinda aliweka wazi nia ya kuelekea Ikulu akisisitiza kuwa hajatangaza rasmi lakini akasema kuwa ameanza harakati hizo
‘kimyakimya’. Alikuwa akijibu moja ya maswali aliyoulizwa katika Kipindi cha Dira ya Dunia kinachorushwa na Shirika
la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Alitamka rasmi kuwania nafasi hiyo baada
ya kuulizwa kuwa anafikiri ni kiongozi
gani anayefaa kurithi mikoba
itakayoachwa na Rais Jakaya Kikwete.
“Mikoba ya Rais Kikwete inaweza
kuchukuliwa na yeyote atakayeonekana
mwisho wa safari kwa utaratibu wa
chama na ndani ya Serikali .... kama
anafaa. Waliojitokeza sasa ni wengi na mimi ninadhani ni vizuri,” alisema Pinda.

Alipoulizwa kama yupo miongoni mwa wengi alisema, “… umesikia kama nimo … basi tukubali hilo na yeye Waziri Mkuu
yumo. Hao wote waliojitokeza pamoja na
Waziri Mkuu aliyejitokeza ni katika
jitihada za kusema hebu Watanzania
nitazameni je, mnaona nafaa au hapana?”
“……..fanyeni hivyo kwa mwingine na
mwingine, mwisho wa yote zile kura
zitakazopatikana kwenye mkutano mkuu
kama ni kutokana na chama kile
kinachotawala na hatimaye Watanzania
watakaojitokeza kupiga kura Oktoba
kutokana na wagombea watakaojitokeza
kutoka kwenye vyama mbalimbali huyo
ndiye tutakayempata kama rais.

Hivyo natangaza nia hiyo kimyakimya.”
Kiongozi huyo atakuwa wa pili kutangaza nia hiyo kupitia vyombo vya habari vya kimataifa, baada ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.

Alitangaza nia hiyo Julai 2, 2014,
alipokuwa Uingereza katika mkutano wa sekta ya mawasiliano baada ya kuhojiwa kwenye kipindi hicho hicho cha Dira ya Dunia.

Soma zaidi Mwananchi

No comments

Powered by Blogger.