Header Ads

FAHAMU; FAIDA YA MASWALI HAYA KWENYE MAHUSIANO YAKO!

Kupendana kwa dhati ni nguzo imara inayofanya mapenzi baina ya wapendanao yaweze kuwa
imara na madhubuti.

Wanaopendana kwa dhati
wanasikilizana, kuhesimiana na kila mmoja kuwa na hamu na shauku na mwenzake. Katika mapenzi hivyo ni vitu muhimu sana. Ili mapenzi yaweze kustawi heshima inabidi iwepo baina ya wahusika. Ili kila mmoja aweze kuwa na furaha na faraja katika mahusiano inabidi
miongoni mwao kuwepo na hamu na shauku. Mmoja akikosa hali hii mapenzi hukosa ladha. Si
ajabu kuona mwingine akianza kuhisi anajipendekeza kwa mwnenzake au kuona
akikosa raha kabisa ndani ya mahusiano hayo.

Wewe uko vipi kwa mpenzi wako?
Je, unampa sababu ya kwenda kifua mbele kwa marafiki zake na kusema anamtu anayempenda
kwa dhati?

Umempa jeuri hiyo mwenzako?
Au ndiyo vile kila siku unamfanya asitamani kuwepo mapenzi katika dunia! Unafanya ajivunie kuwa katika mahusiano kama
wenzake anavyowasikia wakisema.

Au umempa manung’uniko na ganzi ya moyo?
Ikiwa hukulazimishwa kuingia katika mahusiano na uliyenaye hupaswi kumfanyia hivyo.

Mapenzi ni faraja na burudani, sasa kwanini unamfanyia hivyo mwenzako?
Hivi ulishawahi kujiuliza hatima ya lawama za kila siku za mpenzi wako dhidi ya matendo yako yasiyoonesha dalili za mapenzi wala kumjali?
Tengeneza picha ya kitakachotokea baada ya mpenzi wako kuchoshwa na hali hiyo. Hakuna
binadamu anayependa kuteseka ikiwa kuna sehemu anahisi atapata faraja na amani ya nafsi.

Je, vipi kauli zako kwa mpenzi wako ni zile za kujenga tabasamu katika sura yake au ni maudhi na fujo kwa kwenda mbele?
Unamfanya mwenzako afurahi karibu kila neno linalotoka
katika kinywa chako, au ndiyo ukianza kuongea tu unamfanya alie na kujutia hatua yako ya kufungua
mdomo?

Maneno yako yanachangia asilimia ngapi ya furaha katika maisha yake?
Au ndiyo asilimia kubwa ya huzuni zake zipo katika maneno yako.

Unampa sababu ya kukuamini?
Au ndiyo ukitoka tu yeye tumbo joto akifikiria kile alichokikuta katika simu yako! Yuko hivyo?
Chunga sana.

Bofya kusoma zaidi; MR. CLEVER

No comments

Powered by Blogger.