Waendesha mashitaka:Pistorius aende jela
Oscar Pistorius akitoka mahakamani,Pretoria,
Afrika Kusini
Waendesha mashitaka wamekuwa wakipanga hoja
zao dhidi ya mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar
Pistorius ili aweze kutumikia kifungo jela kwa
kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Shahidi wa kwanza upande wa mashitaka katika
kikao cha kusikiliza hukumu alikuwa Kim Martin,
binamu yake Bi Steenkamp.
Pistorius alipatikana na hatia ya kumuua bila
kukusudia Bi Steenkamp mwezi uliopita - lakini
aliondolewa mashitaka ya kuua kwa kukusudia.
Wakati huo huo familia ya Steenkamp imetoa
taarifa mpya ikisema hawahitaji pesa kutoka kwa
Pistorius.
Kikao cha kusikiliza hukumu kimeahirishwa
Jumatano na kinatarajiwa kuendelea Alhamisi.
Post a Comment