Header Ads

MECHI YA SIMBA NA YANGA, SIMBA YAINGIZA SH MILIONI 427


Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
MPAMBANO wa Ligi Kuu ya soka ya
Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara
kati ya watani wa jadi, Yanga na Simba
uliochezwa juzi (Oktoba 18 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeingiza
sh. 427,271,000.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bila
kufugana.
Mashabiki 49,542 walikata tiketi kushuhudia
mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh.
7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 65,176,932 wakati
asilimia 5 ya gharama ya tiketi kwa CRDB ni
sh. 21,363,550.

Kwa upande wa Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) ambayo ni sh. 1,000
kwa kila tiketi, timu mwenyeji Yanga imepata
sh. 17,339,700, Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
7,431,300 na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) sh. 24,771,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni Uwanja
sh. 43,678,277.67, gharama za mchezo sh.
24,751,024.01, Bodi ya Ligi sh.
23,295,081.42, TFF sh. 17,471,311.07, DRFA
sh. 10,191,598.12, timu mwenyeji Yanga sh.
100,460,038.64 na timu ngeni Simba sh.
71,341,186.86.

No comments

Powered by Blogger.