Header Ads

TAMKO RASMI LA SERIKALI KUHUSU TETESI ZA KUWA NA MGONJWA MWENYE EBOLA NCHINI!

         Utangulizi
Mnamo tarehe 18 Oktoba 2014, Wizara
ilipokea taarifa kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza ya kuwepo kwa
mgonjwa aliyehisiwa kuwa na ugonjwa wa
Ebola. Mgonjwa huyu aliyekuwa na umri wa
miaka 17, jinsia ya Kike na mkazi wa kijiji
cha Bupandwa Tarafa ya Kahunda Wilaya ya
Sengerema, alilazwa akiwa na dalili za homa
kali, manjano, kutokwa na damu sehemu
mbalimbali za mwili.
Mgonjwa huyu alilazwa katika Kituo cha Afya
Mwangika tarehe 15 hadi 16 Oktoba, 2014
ambapo pia alionekana kuwa vimelea vya
ugonjwa wa Malaria kabla ya kuhamishiwa
Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema
mnamo tarehe 17 oktoba 2014 na kufariki
duniani siku hiyo hiyo muda wa saa 3.30
usiku.
Hata hivyo, mgonjwa huyu hakuwa na
historia ya kusafiri kwenda nchi
zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola na
hakuwahi kupokea mgeni kutoka nchi hizo
ndani ya siku ya 21 zilizopita.
Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na;

i.Sampuli ya damu ya mgonjwa kwa ajili ya
uchunguzi wa Kimaabara ilipokelewa tarehe
18 Oktoba, 2014. Matokeo ya awali dhidi ya
magonjwa ya jamii ya ebola yakiwa ni
pamoja na Dengue na Chikungunya
yanaonyesha kuwa mgonjwa hakuwa na
magonjwa haya. Uchunguzi wa kimaabara
bado unaendelea na Wizara itatoa taarifa
rasmi pindi utakapokamilika.

ii.Mgonjwa alihudumiwa katika chumba
maalumu kilichotengwa ambapo wahudumu
pamoja na walioshughulikia mazishi yake
walivaa vifaa kinga (PPE)

iii.Wataalamu pamoja na ndugu
waliomhudumia mgonjwa kabla ya mauti
kumfika wametengwa na wapo kwenye
uangalizi maalumu
Mwongozo wa utambuzi wa ugonjwa huu
(Standard Case Definition) unaeleza kwamba
ili mgonjwa aweze kuhusiwa kuwa na
ugonjwa wa Ebola anatakiwa akidhi vigezo
ifuatavyo:

i. Dalili za awali ni homa kali ya ghafla,
kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuumwa
na kichwa, na kutokwa na vidonda kooni.
Mara nyingi dalili hizi hufuatiwa na
kutapika, kuharisha,kutokwa na vipele vya
ngozi, kwa baadhi ya wagonjwa hutokwa na
damu ndani na nje ya mwili

ii.Awe amesafiri kwenda sehemu
zilizothibitishwa kuwa na ugonjwa wa ebola
ndani ya kipindi cha wiki 3

iii. Kugusa majimaji kutoka kwa mgonjwa,
maiti au mnyama anayehisiwa au
kuthibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.
HitimishoWizara inapenda kuwatoa hofu
wananchi kuwa hadi sasa HAKUNA MGONJWA
yeyote aliyethibitishwa kuwa na virusi vya
ugonjwa wa Ebola hapa nchini. Hata hivyo
uchunguzi wa kina wa Kimaabara unaendelea
na taarifa itatolewa baada ya majibu
kupatikana.

No comments

Powered by Blogger.