Header Ads

6 WAFARIKI KWA AJALI YA MTUBWI NA WENGINE 27 KUOKOLE - ZIWA TANGANYIKA


UPDATES: WATU 27
WAMEOKOLEWA AJALI YA
MTUMBWI ZIWA TANGANYIKA, 6
WAMEFARIKI
Na Mwajabu Hoza Kigoma.
WATU sita wamekufa 27 wameokolewa na
wengine 11 kulazwa katika hospitali ya rufaa
maweni iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani
Kigoma baada ya boti walilokuwa wakisafiria
kuzama katika ziwa Tanganyika mkoani humo.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari
kamishina msaidizi wa polisi mkoa kamanda Jafar
Mohamed alisema tukio hilo limetokea majira ya
saa nne asubuhi katika kijiji cha Kalalangabo
kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika kwenye
halmashauri ya wilaya Kigoma.
Kamanda Mohamed alisema chanzo cha tukio hilo
ni idadi kubwa ya watu waliokuwa katika boti hilo
na kusababisha kuzama majini mita 200 kutoka
nchi kavu na kwamba watu hao walikuwa
wakielekea kwenye sherehe ya harusi katika kijiji
cha Kigalye kilichopo jimbo la Kigoma Kaskazini
mkoani humo.
Alisema watu waliopatikana ambao ni marehemu
ni watu sita wakiwemo watoto wawili kati ya hao
mmoja ametambuliwa kwa jina la Salama Juakali
(37) huku wengine majina yao yakiwa hayaja
tambuliwa hadi sasa.
Kamanda amesema hatua za uokoaji zinaendelea
sanjari na taratibu za kuhakikisha waliohusika na
tukio hilo wanafikishwa katika vyombo vya sheria
kujibu tuhuma inayowakabili.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa wavuvi
katika mwalo wa Kibirizi uliopo Manispaa ya
Kigoma Ujiji Sedwe Ibrahimu alieleza idadi ya
watu waliozama majini inasadikiwa kuwa zaidi ya
watu 64 ambao walikuwa wakielekea harusini.
Alisema mitumbwi iliyosababisha ajali ilikuwa
miwili ambayo ni maalum kwa kuvulia samaki na
dagaa hivyo ilitumika kusafirishia abiria baada ya
kukodiwa kwa lengo la kuwfikisha maharusi katika
kijiji cha Kigalye wakitokea katika kijiji cha
Mwandiga jimbo la Kigoma Kaskazini ndipo
walipokutwa na janga hilo.
Akifafanua kuhusu tukio hilo baada ya kupatiwa
tarifa ya kuzama kwa mitumbwi miwili iliyokuwa
imebeba watu waliokuwa katika magari matatu
aina ya Hiace pamoja bodaboda tatu kiasi
ambacho kinaashiria watu hao walikuwa wengi
ukilinganisha na uwezo wa mitumbwi hiyo
ambayo hubeba watu 20 tu wakati wa shughuli za
uvuvi.
Alieleza eneo ambalo walitumia kupakia abiria hao
ilikuwa katika kijiji cha Kalalangabo ambapo si
rasmi kwa kupakia abiria kisheria na hivyo
kutakiwa kutumia eneo la kibirizi ambalo
limetengwa kisheria.
Baaadhi ya wahanga wa tukio hilo akiwemo
Zainabu Issa na Mariamu Juma (18) ambaye ni
bibi harusi alisema chanzo ni baada ya mitubwi
hiyo kukumbwa na wimbi la maji sambamba na
idadi kubwa ya watu takribani 80 ambao walikuwa
katika mitumbwi hiyo.
Muuguzi wa zamu katika wodi namba tano Haika
Masula alisema wamepokea majuruhi 10 na maiti
tatu mwanamke mmoja alitambuliwa kwa jina la
Salama Juakali na watoto wawili waliochini ya
umri wa miaka mitano.

No comments

Powered by Blogger.