TANZANIA YAPANDA JUU TANO VIWANGO VYA FIFA MWEZI HUU!
SOKA YA TANZANIA YAPAA MATAWI YA JUU FIFA, UGANDA
NA KENYA WOTE WAPOROMOKA,
UJERUMANI BADO NAMBA MOJA
DUNIANI, ALGERIA YAONGOZA WAAFRIKA WOTE
TANZANIA imepanda kwa nafasi tano katika viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) hadi nafasi ya 110 kwa mwezi huu.
Takwimu za mwezi huu zilizotolewa na FIFA leo, zinaonyesa Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 115 mwezi uliopita kwa kufikisha pointi 291, wakati Kenya imeporomoka kwa nafasi tano hadi ya 116, Uganda imeendelea kuwa juu ya nchi zote wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), pamoja na kushuka kwa nafasi tano hadi ya 84.
Ujerumani bado inaongoza kwa ubora wa soka duniani, ikifuatiwa na Argentina, Colombia, Ubelgiji, Uholanzi, Brazil, Ufaransa, Uruguay, Ureno na Hispania katika kumi bora.
Algeria imepanda kwa nafasi tano hadi ya 15 duniani na sasa ndiyo nchi ya Afrika inayoongoza kwa ubora wa soka, wakati Ivory Coast imeshuka kwa nafasi tatu zaidi hadi ya 25, Ghana imeshuka kwa nafasi mbili hadi ya 35, wakati Misri imepanda kwa nafasi 23 hadi ya
38 na Cameroon imepanda kwa nafasi mbili hadi ya 40, ikifuatiwa na Senegal na Nigeria ambazo zote zimeporomoka kwa nafasi tano.
Kupanda kwa Tanzania nafasi tano mwezi huu, wazi kumetokana na ushindi wa 4-1 dhidi ya Benin katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Oktoba 12 Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, Kipigo hicho kimepeleka athari kubwa kwa Benin, ambayo sasa inaporomoka kwa nafasi nane hadi 86.
Post a Comment