KOVA AKANUSHA UTEKWAJI WA WATOTO DAR ES SALAAM
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam limekanusha vikali uvumi
unaoendelea kuzushwa jijini Dar es Salaam
kuhusu utekeaji nyara wa watoto wadogo
wanaosoma shule za jiji hilo na kuwataka
wananchi kuupuuza.
Akizungmza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ,
alisema kuwa mpaka sasa jeshi hilo halina
taarifa yoyote ya mtoto kutekwa au
kufanyiwa madhara yoyote kwa mtindo wa
utekaji nyara.
“ Jeshi la Polisi limegundua kwamba huu ni
uvumi ambao haujulikani chanzo chake
hivyo wananchi wanaombwa kuachana nao
na kuupuza kwani unaleta hofu katika jamii
bila sababu za msingi ” alisema Kova .
Alisema kuwa pia uvumi huo umeanza
kuleta usumbufu ambapo mnamo Oktoba 3
mwaka huu saa 3: 00 asubuhi huko
Vingunguti , mtu mmoja aitwaye Prosper
Makame (34 ) akiwa na mkewe Marystella
Munis (30 ) walipata usumbufu unaotokana
na uvumi huo .
Kamishna Kova aliongeza kuwa watu hao
ambao ni wafanyabiashara wa vyombo vya
nyumbani walifika maeneo ya shule ya
msingi Kombo iliyopo Vingunguti kwa ajili
ya biashara zao , wakiwa na gari aina ya
Noah yenye namba T 252 DAY , ghafla
walizingirwa na watu wakidaiwa wanateka
wanafunzi .
“ Pia mnamo Oktoba 13, 2014 majira ya saa
4 : 00 asubuhi huko katika kituo cha Polisi
Tabata uliibuka uvumi kuwa gari namba
T548 BUN aina ya Noah rangi nyeusi ambayo
ni mali ya askari polisi A/ INSP Ester wa
kikosi cha usalama barabarani , ilivumishwa
kwamba ndani ya gari hiyo kuna vichwa
vitano vya watoto wa shule ya msingi
Mtambani na kusababisha wazazi wenye
watoto wanaosoma shule hiyo kukusanyika
kituoni hapo ili kushuhudia na kuona
vichwa hivyo ” alisema Kamishna Kova na
kuongeza:
“ Na ndipo Mkuu wa kituo hicho cha Polisi
aliamuru gari hilo lifunguliwe na
kuwathibitishia wananchi kuwa habari hizo
ni za uongo na uvumi”
Kutokana na tukio hilo jeshi hilo lilifanya
uchunguzi na kumkamata mtu mmoja
Gilbert Stanley (32 ) mhehe mkulima na
mkazi wa Tabata alipohojiwa alikiri
kueneza habari hizo na kudai yeye
aliambiwa na mtu ambaye hakumkumbuka .
Hivyo , Kamishna Kova alisisitiza kuwa
uvumi wa kuwepo kwa kikundi cha wahalifu
wanaowateka watoto wanafunzi si wa kweli
hata kidogo na hivyo wananchi wanatakiwa
kuepukana na taarifa hizo kwani zinaweza
kusababisha uvunjifu wa amani.
Katika hatua nyingine , Kamishna Kova
alithibitisha kutokea kwa vifo vya watu
watano na wengine 16 kujeruhiwa katika
ajali ya moto iliyotokea Oktoba 13 mwaka
huu majira ya saa 5: 00 usiku huko kwenye
mzunguko wa Mbagala Charambe baada ya
lori aina ya Scania T347 BXG lilipoanguka
likiwa na mafuta aina ya petrol lita 38, 000.
Aliwataja waliofariki kuwa ni Masoud
Masoud mkazi wa Charambe , Hassani
Mohamed mkazi wa Mbagala Kibangulile ,
Mohamed Ismail , Ramadhani Halfan na
Maulidi Rajabu wote ni wakazi wa Mbagala
Charambe .
Alisema kuwa majeruhi wamelazwa kwenye
hospitali ya taifa ya Muhimbili na hospitali
ya wilaya ya Temeke wakiendelea na
matibabu huku ajali hiyo pia ikisababisha
nyumba ya kulala wageni iitwayo United
kuungua moto na kuteketea kwa pikipiki
saba za bodaboda zilizokuwa zimeegeshwa
karibu na aneo hilo, maduka matano yenye
bidhaa zenye thamani ya shilingi Milioni 197
yaliungua moto .
Kamishna Kova aliwataka wananchi kuacha
tabia ya kukimbilia kwenye ajali za magari
ya mafuta kwani ni hatari kwa maisha yao
kwani watu wengi waliojeruhiwa walikuwa
wakichota mafuta yaliyomwagika
kutokanana ajali hiyo .
Katika tukio lingine , Kamishna Kova alisema
kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kumkamata
jambazi sugu aitwaye Paulo Thamas Milanzi
maarufu Chinga (35) mmakonde mkazi wa
Chanika ambaye baada ya majibizano ya
risasi jambazi hilo lilijeruhiwa na kufikshwa
hospitali ya muhimbili kwa matibabu
ingawa baadaye alifariki dunia.
Alisema jambazi hilo lilikuwa likitafutwa na
polisi kutokan na kuhusika kwenye matuio
ya mauaji na wizi ikiwemo tukio la kuuawa
kwa Afisa Mwandamizi wa Usalama wa
Taifa , Sylivabus Adrian Mzeru Aprili 29
mwaka huu liliotokea Uwanja wa Ndege.
Aliongeza kuwa jambazi lilikamatwa na
bastola aina ya Star ambapo majambazi
wenzake walikamatwa na sasa wako
gerezani , hivyo ameitahadharisha jamii
iachane na uhalifu kwani hauna manufaa
yoyote.
Post a Comment