Header Ads

CHADEMA WACHAPANA MAKONDE WAKIFANYA UCHAGUZI - KAHAMA

Siasa Bwana !! CHADEMA
WACHAPANA MAKONDE WAKIFANYA UCHAGUZI - KAHAMA

Uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA,wilaya  ya Kahama
mkoani Shinyanga umeingia dosari,baada
ya mmoja wa madiwani wa chama hicho
kuhusishwa na rushwa na vitendo vya
usaliti ndani ya chama kutoka CCM.

Pia katika uchaguzi huo baadhi ya
wagombea wamechapana makonde
baada ya kuenguliwa kwa baadhi ya
majina ya wagombea katika uchaguzi wa
Baraza la Vijana wa chama hicho
(BAVICHA),huku Red Brigade wakihusika
katika vurugu hizo.

Hali hiyo ilitokea juzi mjini Kahama katika
ukumbi wa Mamba Hall, baada mgombea
wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho
wilayani Kahama Leonard Mayala ambaye
pia ni Diwani wa Kata ya Nyasubi,
alienguliwa kuwania nafasi hiyo baada ya
kubainika kutumia rushwa kuomba
achaguliwe katika nafasi hiyo.

Mgombea huyo alituhumiwa kutumia
shilingi milioni mbili kuwahonga baadhi
ya wanachama,fedha ambazo zinadaiwa
zilitolewa na baadhi ya makada wa
Chama cha Mapinduzi kwa njia ya
mtandao wa (Mpesa)ili kuhakisha
ananyakuwa nafasi hiyo.

Tuhuma hizo zimekuja baada ya
wanachama kutokuwa na imani naye
kutokana na mwenendo wa diwani huyo
wa kuwa karibu na makada wa CCM
wilayani hapa na hivyo kusababisha
viongozi na wasimamizi wa uchaguzi huo
kuengua jina lake  baada ya kuridhika na
ushahidi uliotolewa na kuwekewa
pingamizi.

Aidha katika uchaguzi huo baadhi ya
wagombea na wanachama walichapana
makonde wakipinga kuenguliwa majina
ya baadhi majina ya wagombea katika
uchaguzi wa Baraza la Vijana wa
Chadema (BAVICHA).

Ugomvi huo ulitokea baada ya wagombea
waliopitishwa katika nafasi ya Uenyekiti
wa Bavicha kuanza kujinadi kwa
wananchama ndipo mgombea Thomas
Masanja aliyeenguliwa katika
kinyang’anyiro hicho kutokana na kukosa
sifa ikiwemo kadi yake ya uanachana
kutotambulika alijitokeza na kuzuia
uchaguzi.

Kufuatia kuenguliwa kwa mgombea huyo
ndipo badhi ya wafuasi wake  wakiwemo
Red Brigade walipojitokeza na kuanza
kufanya fujo kwa lengo la kuzuia
uchaguzi huo kuendelea wakidai kwamba
mgombea wao kutotendewa haki kwa
kuenguliwa kinyemela kugombea nafasi
hiyo.

Hali hiyo ilikwenda mbali zaidi  kwani
wafuasi hao walianza kuwashambulia
baadhi ya viongozi na wasimamizi
ambapo Mwenyekiti wa Chadema wa
Halmashauri ya Msalala Emmanuel
Bombeda alipigwa ngumi na Red brigade
waliokuwa wakimuunga mkono
mgombea aliyeenguliwa.

Utulivu na amani urejea ukumbini humo
baada ya msimamizi wa uchaguzi wa
Chama hicho kanda ya Ziwa
Mashairiki,Madata Sande kuingilia kati na
kuwataka wanachama kuwa wavumilivu
ili kufanikisha uchaguzi huo kwani
wagombea walioenguliewa katika
kinyang’anyiro hicho walienguliwa
kihalali bila upendeleo wowote kwa
kuzingatia katiba ya chama hicho.

Katika uchaguzi huo wajumbe
walimchagua Juma Protas,kuwa
Mwenyekiti wa  Chadema wa wilaya
hiyo,naye Mshibu Peter akiteuliwa
kushika nafasi ya Ukatibu wa chama
hicho,nafasi ya Ukatibu Uenezi
ikimwangukia Anord Peter na Mweka
Hazina alichaguliwa,Elias Mayunga.

Nalo Baraza la Vijana BAVICHA
lilimchagua Samwel Peter kuwa
Mwenyekiti wake na ndani ya uchaguzi
huo wajumbe walichagua viongozi mbali
mbali wa yakiwemo mabaraza ya
Wazee,Wanawanake na wajumbe wa
mkutano mkuu taifa wa chama hicho.

source; Mohabmatukio blog

No comments

Powered by Blogger.