MAMENEJA WA T.I KUTOA SEMINA YA MUZIKI - DAR
T.I akiwa na manager wake Jason Geter
Ikiwa ni siku chache tu zimebakia ili
shangwe za Serengeti Fiesta zitawale katika
maskio ya wakazi wa Dar es Salaam, October
18, Meneja wa T.I., Jason Geter pamoja na
meneja wa Wizkid na Waje, Cecil Hammond,
wanatarajia kutoa semina kwa wadau wa
muziki itakayofanyika ijumaa hii.
Akizungumza Mtandao huu leo
mwenyekiti wa tamasha la Serengeti Fiesta
2014, Sebastian Maganga, amesema meneja
wa T.I. na yule wa Waje wanatarajia kuingia
Jumatano, October 15 ili kujiandaa na
shughuli mbalimbali ikiwemo semina pamoja
na kufungua duka litakalouza kazi za T.I.
“Mpaka sasa ratiba inaenda vizuri, meneja wa
T.I ‘Jason Geter’ na meneja wa Waje na
Patoraking, wanatajia kuingia usiku wa
Jumatano, kwa sababu kama meneja wa T.I.
anakuja mapema ili kuangalia mazingira na
atakuwa na semina na wadau wa muziki
kuzungumzia jinsi muziki au msanii
unavyoweza kutumia jina lako kibiashara.
Pia atafungua duka ambalo litakuwa linauza
productiob za T.I. Pia meneja wa Waje ‘Cecil
Hammond’ atakuwepo kwenye semina hiyo,”
alisema Sebastian Maganga.
Cecil Hammond
Pia Sebastian alisema wasanii wa kimataifa
wanaotarajia kupagawisha kwenye jukwaa la
Serengeti Fiesta ni T.I, kutoka Marekani,
Waje na Patoraking kutoka Nigeria pamoja na
Victoria Kimani kutoka Kenya. Pia amedai
kuna msaani mmoja mkubwa kutoka Nigeria
ambaye bado wapo kwenye mazungumzo na
jibu ramsi litapatikana kesho mchana.
“Katika wasanii wa kimataifa T.I. ataingia
Dar Ijumaa usiku,” amesema.
Wasanii wa Bongo wanaotarajia kupanda
jukwaa moja na wakali hao kutoka nje ni,
Diamond, Alikiba, Ommy Dimpoz, Mr Blue,
Stamina, Nay wa Mitego, Vanessa Mdee,
Mwana FA, Weusi,Young Killer Msodoki,
Linah Sanga, Recho, Barakah Da Prince, Mo
Music, pamoja na Super Nyota G.Luck, K.
Style pamoja na Edu Boy.
CDT:BONGO 5
Post a Comment