Header Ads

DIVIDO NA UONGOZI WA CLOUDS FM KUBURUZWA MAHAKAMANI, KWA KUKAIDI AMRI YA MAHAKAMA - TIMES FM

TIMES FM KUWABURUZA
MAHAKAMANI DAVIDO NA
UONGOZI WA CLOUDS FM KWA
KUKAIDI AMRI YA MAHAKAMA

KITUO cha redio cha Times FM na kampuni
ya Times Promotions, wamewasilisha
mashtaka mahakamani ya kutaka viongozi
wa juu wa Clouds FM pamoja na msanii wa
Nigeria, Davido wapelekwe jela baada ya kukaidi
amri ya mahakama.

Kampuni hiyo kupitia
wakili wake Peter Kibatala imewasilisha
mashtaka hayo katika mahakama ya
hakimu mkazi ya Kisutu jijini Dar es
Salaam Jumatatu hii.
Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Davido na
Clouds FM walikaidi amri ya mahakama
iliyotolewa kumtaka Davido asitumbuize
kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika
October 18 kwenye viwanja vya Leaders
jijini Dar es Salaam.

Times FM walikuwa wameshaingia mkataba
na Davido atumbuize November 1 kwenye
tamasha lao ambalo linadaiwa
kuahirishwa kutokana na kilichotokea.
Soma zaidi habari hiyo iliyoandikwa
kwenye gazeti la leo la Daily News

No comments

Powered by Blogger.