Header Ads

Kanye West azikataa shilingi bilioni 7.5 kutumbuiza kwa siku 9 jijini Las Vegas

Kanye West amekataa ofa ambayo ingemfanya kuwa mtumbuizaji anayelipwa fedha nyingi zaidi jijini Las Vegas.

Mtandao wa TMZ umedai kuwa Yeezy amekataa kulipwa dola milioni 4.5 (zaidi ya shilingi bilioni 7.5) kwa kazi ya siku 9 peke yake.

Yeezy angetumbuiza show tatu kila wiki kwa kipindi cha wiki tatu kwenye kiota cha Planet Hollywood. Alikuwa $500,000 kwa show moja.

J-Lo ana ofa ya $350K kwa show moja, Britney, analipwa $475K/show na Celine Dion, analipwa $476K kwa show moja kwenye kiota hicho.

No comments

Powered by Blogger.