Header Ads

LIVERPOOL YAUA 3-2, MABAO MAWILI QPR WAJIFUNGA, BALOTELLI LIVERPOOL ACHEKA NA NYAVU MITA TATU


LIVERPOOL imeshinda 3-2 dhidi ya Queens
Park Rangers jioni ya leo katika mchezo wa
Ligi Kuu ya England Uwanja wa ugenini.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Richard
Dunne aliyejifunga dakika ya 67, Philip
Coutinho dakika ya 90 na Steven Caulker
aliyejifunga pia dakika hiyo hiyo ya 90.
Richard Dunne leo ameweka rekodi ya kuwa
mchezaji wa kwanza kujifunga mabao 10
katika historia ya Ligi Kuu ya England.
Raheem Sterling alianza leo kwenye kikosi
cha Liverpool na kocha wa England, Roy
Hodgson akamshuhudia kutokea jukwaani.
Mario Balotelli alikosa bao akiwa amebaki
yeye na nyavu, baada ya kupiga juu akiwa
umbali wa mita tatu wakati huo matokeo bado
yapo sare.

No comments

Powered by Blogger.