Header Ads

Joto uchaguzi Serikali za mitaa lapanda

Dar es Salaam. Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi) imetangaza ongezeko la idadi
ya kata, vijiji, mitaa na vitongoji nchini
vitakavyotumika kwa ajili ya uchaguzi
serikali za mitaa, huku hatua hiyo ikiibua
hoja miongoni mwa wanasiasa na
wasomi.
Tayari vyama vya siasa vimeanza kufanya
maandalizi ya uchaguzi huo wa serikali za
mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba
14, mwaka huu. Wanasiasa na wasomi
wametoa maoni yao kuhusu hatua hiyo,
wengi wakilalamikia jinsi isivyokidhi
mahitaji ya wananchi na wengine
wakielezea kuwa imetangazwa wakati
huu kuwanufaisha wachache ili wapate
madaraka.
Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi
wa Serikali za Mitaa Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kalist Luanda alisema Serikali imeongeza
idadi hiyo ili kuanzisha maeneo mapya ya
kiutawala ambayo yatawawezesha
wananchi kupata huduma za kijamii na
kiutawala kwa karibu.
Alisema ongezeko hilo limefanywa kwa
kuzingatia idadi ya watu kuongezeka kwa
kasi na kupanuka kwa maeneo baada ya
watu kujisajili, hivyo kata zimeongezwa
na kuwa 465, vijiji 628, mitaa 746 na
vitongoji 4,257. Kata kwa nchi nzima
zimeongezwa kutoka 3,802 mwaka 2009
hadi 3,337, vijiji vimeongezeka kutoka
11,795 hadi 12,423 na mitaa imetoka 2,995
hadi 3,741 kwa upande wa vitongoji
imeongezeka kutoka 60,359 hadi 64,616.
Nape
Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape
Nnauye akizungumzia uamuzi huo
aliikosoa hatua hiyo akieleza kwamba
idadi ya vijiji vilivyoongezwa ni ndogo
ikilinganishwa na mahitaji yaliyopo.

MWANANCHI

No comments

Powered by Blogger.