BENKI KUU 'BOT' YAANZA KUCHUNGUZA NOTI YA SH 1000, KUFUATIWA NA MALALAMIKO KUKOSEWA KWA PICHA YA BABA WA TAIFA
BENKI KUU 'BOT' YAANZA KUCHUNGUZA NOTI YA SH 1000, KUFUATIWA NA MALALAMIKO KUKOSEWA KWA PICHA YA BABA WA TAIFA
Kumbukumbu zako ziko sawa kuhusu yale malalamiko ya kukosewa kwa picha ya baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere kwenye noti ya shilingi elfu moja? basi kama hazipo sawa, ichukue hiyo.
Baada ya hayo malalamiko unaambiwa Benki Kuu ya Tanzania imesema imeanza kufanyia kazi malalamiko ya kukosewa kwa picha ya Rais wa kwanza wa Tanzania, Marehemu Mwalimu Julius Nyerere ambapo mkurugenzi wa huduma za kibenki Emmanuel Boaz amesema tayari benki hiyo imeanza kufanyia kazi hayo malalamiko baada ya kusoma katika mitandao ya jamii.
Mwananchi wameandika mkurugenzi huyo alisema BoT haijapata taarifa rasmi kutoka kwa
mtu yoyote lakini wameamua kuzifanyia kazi taarifa hizo >>> “Na sisi tumesoma katika
mitandao, hakuna taarifa rasmi tuliyoipata lakini hatuwezi kudharau tuhuma hizo na endapo tukigundua kuna matatizo tutachukua hatua za
kubadilisha haraka” Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, suala la picha kukosewa sio geni kwani ilishawahi kutokea mara kadhaa kwa marais wastaafu na BoT ililazimika kubadili haraka ili kutoharibu mtazamo wa Taifa ambapo alitoa mfano wa picha ya Mwalimu Nyerere kukosewa na kuonekana nguo aliyovaa imefanana na blauzi lakini pia picha ya Rais Ally Hassani Mwinyi ambayo ilionekana shingoni ana mikunjo.
Kutokana na hali hiyo, mkurugenzi huyo aliwatoa hofu Watanzania kuwa endapo itabainika kama noti hizo zina kasoro zitarekebishwa ambapo hivi karibuni, mitandao ya kijamii iliwakariri wanafamilia ya Rais huyo wa kwanza wakilalamikia picha hiyo kwenye noti ya Sh1,000 kukosewa.
Post a Comment