Header Ads

Boko Haram wateka wanawake wengine

Taarifa kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, zinasema kuwa idadi kubwa ya wanawake wengine wametekwa nyara na kundi la wapiganaji la Boko Haram.

Wiki jana maafisa wakuu wa nchi hiyo walitangaza kufikia makubaliano ya kusitisha vita na kundi hilo.

Kwa hiyo kundi hilo lilikubali kuwaachilia wasichana zaidi ya mia mbili waliotekwa na kundi hilo kama sehemu ya makubaliano hayo miezi sita iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakazi wa eneo hilo, wapiganaji wa Boko Haram walishambulia vijiji
viwili katika jimbo la Adamawa - Waga Mangoro na Garta. Kisha wakawateka wasichana na wanawake wengi.

Vijiji hivi vinapakana na miji ya Madagali na Michika ambayo imekuwa chini ya udhibiti wa wapiganaji hao kwa wiki kadhaa.

Soma zaidi; BBC

No comments

Powered by Blogger.