Header Ads

VAN PERSIE AINUSURU MAN UNITED KUZAMA KWA CHELSEA, PICHA ZAIDI HAPA!

BAO la Robin van Persie dakika ya mwisho limeipokonya tonge mdomoni Chelsea baada ya Manchester United kupata sare ya 1-1 katika Ligi Kuu ya England jioni ya leo.

United walipata bao hilo la kusawazisha baada tu ya beki Branislav Ivanovic kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Old Trafford, mkongwe Didier Drogba alitangulia kuifungia Chelsea dakika 53 kabla ya Mholanzi, Van Persie kumuokoa Louis Van Gaal na kipigo.

No comments

Powered by Blogger.