Header Ads

MAN UNITED YAMTAKA VALDES, BAADA YA KUIGOMEA LIVERPOOL

BAADA YA KUIGOMEA LIVERPOOL,
SASA MAN UNITED YAMTAKA
VALDES

Baada ya kipa wa zamani
wa Barcelona kugoma kufanya majaribio Liverpool, sasa Manchester United imeanza mazungumzo naye ili ikiwezekana atue Old Trafford.

Victor Valdes ,32, aligoma kufanya majaribio ya siku nne kama Liverpool walivyokuwa wametaka.

Aidha,  Man United kupitia kocha wake, Louis van Gaal wameanza naye mazungumzo.

Kipa huyo aliyechwa na Barcelona sasa yuko huru hivyo haitakuwa gharama kubwa kumpata.

Hata hivyo, kama atakubali kujiunga
na Man United, timu ya tiba ya klabu hiyo ndiyo itaendelea kumsimamia hadi atakapokuwa fiti kiafya.

No comments

Powered by Blogger.