Header Ads

RONALDO ACHANA NAYE, APIGA MBILI REAL IKIUA 5-0 LA LIGA

KLABU ya Real Madrid imeifumua mabao 5-0
Levante na kusogea nafasi ya pili kwenye
msimamo wa La Liga, ikizidiwa pointi nne na
vinara, Barcelona
Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo
alifunga mabao mawili, kwanza la penalti
dakika ya 13 na la tatu dakika ya 61, sasa
akifikisha mabao 15 msimu huu katika ligi
hiyo baada ya mechi mechi saba.
Mabao mengine ya Real, yamefungwa na
Javier Hernandez ‘Chicharito’ dakika ya 38,
James Rodriguez dakika ya 66 na Isco dakika
ya 82.
Kikosi cha Real kilikuwa; Casillas, Carvajal,
Pepe, Nacho, Marcelo/Arbeloa dk73,
Rodriguez, Modric/Medran dk79, Kroos/
Illarramendi dk68, Isco, Hernandez na
Ronaldo.

No comments

Powered by Blogger.