Header Ads

Ajali Yaua Watu 9, baada ya Hiace Kugongana Uso kwa Uso na Lori la Mafuta - Arusha

Ajali mbaya eneo la Tengeru kuelekea Usa, kati ya lory na gari dogo la abiria (hiace) watu kadha wamefariki na majeruhi ni wengi.

Mmoja wa mashahidi aliyefika eneo
la tukio na hospitali ya Mount Meru
amesema ajali ilitokea majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadec Darajani -Tengeru iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace linalobeba watu toka Usa-River kwenda Arusha
mjini na Lori la mafuta.

Watu 9 wamefariki na wengine 2 wamejeruhiwa baada ya basi dogo la abiria Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na lori mafuta katika eneo la Usa River, Arusha.

Aliongeza kuwa chanzo cha ajali
hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa
hiace (gari la abiria) iliyokuwa
ikijaribu kupita magari mengine
ndiyo akakutana uso kwa uso na
lori hilo.

Source; RADIO ONE STEREO

No comments

Powered by Blogger.