KIJANA ALIYEJIUNGA NA IS ATOA ONYO KWA MAREKANI
Kijana raia wa Australia, Abdullah Elmir ' Abu
Khaled' aliyejiunga na kundi la wapiganaji wa
IS wanaopigana nchini Iraq na Syria
ameonekana kwenye kanda ya video .
Katika kanda hiyo kijana huyo mwenye umri
wa miaka 17 anawahutubia waziri mkuu wa
Australia Tony Abbot pamoja na Rais wa
Marekani Barack Obama .
Kijana huyo alisema " hatutasalimisha silaha
zetu hadi tutakapofika katika ardhi yenu . ''
Alitoroka kutoka nyumbani Australia mwezi
Juni na kijana mwingine raia wa Australia na
inaaminika alisafiri kwenda Syria kupitia
Uturuki .
Msemaji wa serikali amesema kanda hiyo ni
idhara ya tishop la kundi la Islam ic State kwa
dunia nzima .
''Na hiyo ndio maana Australia imejiunga na
muungani wa wanjeshi wanaopigana dhidi ya
ISIL nchini Iraq, '' alisema msemaji huyo.
Katika kanda fupi ya video iliyowekwa kwenye
mtandao, Abdullah Elmir waliwahutubia
viongozi hao kwa kusema : ''Kwa viongozi , kwa
Obama , kwa Tony Abbott nasema hivi , hizi
silaha tulizo nazo , wanjeshi hawa hatutakoma
kupigana , hatutasalimisha silaha zetu hadi
tutakapofika katika ardhi yenu . ''
" Hadi tutakapoweka bendera nyeusi katika
kasri ya Buckingham Palace, una hadi
tutakapoweka bendera yetu katika Ikulu ya
Marekani , hatutasitisha vita , '' alisema kijana
huyo mwenye umri wa miaka 17.
Post a Comment